Munich,Ujerumani.
Kiungo wa Bayern Munich Muhispania Thiago Alcantara ameziita kuwa ni uzushi mkubwa taarifa zilizoenea kuwa ataungana na Pep Guardiola katika klabu ya Manchester City msimu ujao.
Leo gazeti la Mundo Deportivo la Hispania limemnukuu Alcantara akiweka wazi kuwa hana mpango wa kuikacha Bayern Munich na kumfuata Guardiola katika klabu ya Manchester City.
Alcantara ambaye aliibuliwa na Guardiola mwaka 2009 kutoka kikosi cha vijana cha FC Barcelona na kisha mwaka 2013 kuungana nae Bayern Munich amesema anapenda kuendelea kuishi Ujerumani.Hana mpango wa kuhama na kama mpango huo ungekuwepo basi asingesaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki Allianz Arena mpaka mwaka 2019.
0 comments:
Post a Comment