Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia
Wambura leo ametembela ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) na kupata kujionea shughuli mbalimbali zinazondeshwa na shirikiso
hilo.
Akiongea na viongozi na wachezaji wa timu ya Taifa ya Wanawake “Twiga
Stars” waliopo kambini kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa
Fainali za Mataifa Afrika kwa Wanawake dhidi ya Zimbambwe, Wambura
amesema Serikali itashirikiana na TFF kuhakikisha timu inapata ushindi
katika mchezo huo wa awali utakaochezwa Machi 4, 2016.
Wambura amewataka wachezaji wa Twiga Stars kuwa na nidhamu ndani na
nje ya uwanja, kujituma na kuiipenda kazi yao hiyo ambayo kwa sasa ni
ajira itakayoweza kuwasaidia kuendesha maisha yao.
Aidha Wambura amesema anaamini kuwa Twiga Stara bado wana nafasi ya
kufanya vizuri katika mchezo unaowakbalili, na kuwaomba kupambana zaidi
kuhakikisha inapanda na kushinda nafasi ya kwanza Afrika katika soka la
wanawake.
Pia amesema wizara yake inashugulikia maombi ya TFF kuiomba wizara ya
TAMISEMI ikasimishe mchezo wa mpira wa miguu katika mashindano ya
UMITASHUMITA na UMISSETA yaweze kusimamiwa na TFF kwani wao ndio wenye
utaalamu wa mchezo huu.
0 comments:
Post a Comment