Manchester,England.
Klabu ya Tottenham Hotspurs imenogesha mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu nchini England baada ya kuibamiza Manchester City kwa mabao 2-1 ugenini.
Mabao yaliyoipa ushindi Tottenham Hotspurs yamefungwa dakika za 59 na Harry Kane kwa mkwaju wa penati baada ya Raheem Sterling kunawa mpira katika eneo la hatari huku bao la pili likifungwa na Christian Erikssen dakika ya 82 akimalizia pasi nzuri ya Erik Lamela.Bao la kufutia la Manchester City limefungwa dakika ya 75 na kinda Kelechi Ihenaicho.
Kufuatia ushindi huo Tottenham Hotspurs imechupa mpaka nafasi ya pili baada ya kufikisha pointi 51 pointi 2 nyuma ya vinara Leceister City wenye pointi 53.
0 comments:
Post a Comment