Mshambuliaji wa kimataifa ya Ivory Coast Salomon Kalou amesema anaona kuna umuhimu wa kuachana na soka la ngazi ya kimataifa.
Mchezaji huyu wa zamani wa Chelsea ameichezea nchi yake michezo 81 na kufunga mabao 29.
Akizungumza
na Bbc kalou amesema" nimeshinda kombe la afrika nimecheza fainali
mbili za kombe la dunia .Lakini nafikiri ni muda sahihi wa kuacha soka
la timu ya taifa ."
"Nitafikisha miaka 30 mwaka huu na ninaanza kufikiria kuhusu kuupumzisha mwili wangu ."
Kalou ameongeza kwa kusema anahisi ni wakati sahihi kuelekeza nguvu zake kwenye klabu yake ya Hertha Berlin.
Mshambuliaji huyu alijiunga na Hertha Berlin mwaka 2014 na kufunga jumla ya magoli sita katika msimu wake wa kwanza
0 comments:
Post a Comment