London,England.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mirror habari zinasema kocha wa Arsenal Mfaransa Arsenal Wenger anafikiria kumteua mlinda mlango Peter Cech kuwa nahodha mpya wa klabu hiyo kufuatia nahodha wa sasa Muhispania Mikel Arteta kuweka wazi kuwa atastaafu mwishoni mwa msimu huu na kugeukia ukocha.
Cech,33 anapigiwa upatu kuwa nahodha mpya kwa msimu kutokana na kuwa na uwezo mkubwa katika nyanja ya mawasiliano.Cech anazungumza lugha tano tofauti kwa ufasaha.Cech ni kiongozi.
Habari zaidi zinadai kuwa Cech pia anabebwa na takwimu kwani tangu atue Arsenal amekuwa kikosi cha kwanza karibu katika michezo yote na hiyo ndiyo sifa inayompa nafasi zaidi ya nahodha msaidizi Per Mertesacker ambaye siku za hivi karibuni amekuwa akiingia na kutoka katika kikosi cha kwanza.
0 comments:
Post a Comment