Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeipongeza timu ya
African Lyon FC ya jijini Dar es salaam kwa kufanikiwa kupanda ligi kuu
ya Vodacom (VPL) msimu ujao, baada ya kuwa vinara wa Kundi A katika ligi
hiyo iliyomalizika jana.
African Lyon imeungana na timu ya Ruvu Shooting FC ya Mlandizi mkoa
wa Pwani iliyokua timu ya kwanza kupanda ligi kuu wiki iliyopita kutoka
kundi B.
TFF inaitakia kila la kheri Africa Lyon FC katika maandalizi ya msimu
mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom, kwa kujiandaa vizuri na mikiki mikiki ya
VPL ambayo ina jumla ya timu 16 na kila klabu kucheza jumla ya michezo
30 kwa msimu nyumbani na ugenini.
0 comments:
Post a Comment