London,England.
SHAMBA LA BIBI!!Hii ndiyo kauli rahisi zaidi unayoweza kuitumia kuhusu mpango wa vilabu vya China kuhusu nyota wa klabu ya Chelsea.Baada ya mwezi uliopita klabu ya Jiangsun Suning kumsajili kiungo Ramires kwa dau la paundi millioni 25 mapema leo hii zimekuja habari nyingine kuwa Loic Remy ametengewa paundi milioni 11 na klabu ya Shaghai Shenhua.
Remy,29 ambaye mwezi januari usajili wake kwenda Leceister City ulikwama dakika za mwisho ameripotiwa kuivutia Shanghai Shenhua kiasi cha kuamua kutangaza nia ya kumsajili pindi tu dirisha la usajili litakopofunguliwa mwezi Mei mwaka huu.
Mbali ya dau hilo la usajili pia Shanghai Shenhua imejipanga kumboreshea Remy mshahara wake mpaka paundi milioni 5.5 kwa mwaka.
0 comments:
Post a Comment