728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, February 27, 2016

    SIASIA AKABIDHIWA MIKOBA YA OLISEH NIGERIA

    Lagos,Nigeria.

    Chama cha soka cha Nigeria [NFF] kimemteua Samson Siasia kuwa kocha mkuu wa timu yake ya taifa kufuatia kujiuzuru kwa aliyekuwa kocha wake Sunday Oliseh mapema jana ijumaa.

    Hii ni mara ya pili kwa Siasia kupata nafasi ya kuinoa Nigeria mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2010 kabla ya mwaka 2011 kutimuliwa kufuatia kushindwa kuipeleka katika fainali za AFCON za mwaka 2012.

    Mbali ya Siasia pia NFF imewateua Salisu Yusuf,Emmanuel Amuneke na Alloy Agu kuwa makocha wasaidizi na jukumu lao kubwa ni kuhakikisha wanaifunga Misri mwezi Machi na kuibuka vinara wa kundi G na hatimaye kufuzu michuano ya AFCON ya mwaka 2017.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SIASIA AKABIDHIWA MIKOBA YA OLISEH NIGERIA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top