London,England.
Kwa mujibu wa gazeti la Sun mmiliki wa Chelsea Mrusi Roman Abramovich atamkabidhi kitita cha £130 millioni kocha mpya ajaye kwa ajili ya kuiimarisha timu hiyo iliyopoteana msimu huu.
Sun linazidi kupasha kuwa Abramovich ametenga kitita hicho akitaka kuongeza sura nne mpya kikosini hapo majira ya kiangazi baada ya kuchoshwa na mwendo mbaya wa timu tangu ilipotwaa ubingwa wa ligi kuu England mwezi Mei mwaka jana.
Sura ambazo tayari zimeanza kutajwa tajwa na huenda zikaletwa na kitita hicho ni Arturo Vidal [Bayern Munich] na John Stones [Everton] kwa ajili ya kuimarisha safu za kiungo na ulinzi.
Kitita hicho pia kimeripotiwa kuwa huenda kikaongezeka maradufu na kufikia £210 millioni ikiwa Eden Hazard atauzwa kwenda Real Madrid wakati wa majira yajayo ya kiangazi.
0 comments:
Post a Comment