London,England.
Kocha wa Arsenal Mfaransa Arsene Wenger amesema mshambuliaji wa klabu hiyo aliyekuwa majeruhi Danny Welbeck atarejea dimbani kwa mara ya kwanza msimuu Februari 20 katika mchezo wa kombe la Emirates FA Cup.
Welbeck,25 amekuwa nje ya dimba tangu mwezi Aprili mwaka 2015 baada ya kuumia goti.Kwa mujibu wa Wenger ni kuwa Welbeck ameshapaona barabara jeraha hilo na atakuwa sehemu ya kikosi kitakachovaana na Hully City katika mchezo wa hatua ya tano ya kombe la Emirates FA Cup.
Mapema wiki iliyopita Welbeck alikichezea kikosi cha U-21 cha Arsenal kwa dakika sitini katika mchezo wa kirafiki.
0 comments:
Post a Comment