Nairobi,Kenya.
Unamkumbuka Michael Olunga yule Straika wa Gor Mahia aliyeifanyia kitu kibaya Yanga katika michuano ya Kagame mwaka jana???
Sasa sikia hii!!Olunga ama Injinia kama wengi wanavyomuita ambaye kwasasa yuko Sweden akifanya majaribio katika klabu ya IF Djurgarden ameweka video kwenye mtandao wa You Tube akimuomba kocha wa Arsenal Mfaransa Arsene Wenger amsajili.
Ujumbe ulioko kwenye video hiyo unasema hivi......
“Habari Arsene Wenger,Mimi ni Michael Olunga Ogada,Straika wa Gor Mahia FC ya Kenya.Kwasasa mimi ndiye mchezaji bora Kenya.Nimefunga magoli 38 msimu uliopita.Ndoto yangu ni kucheza Arsenal.
"Nina kipaji kikubwa na umri wangu ni miaka 21 niko tayari kucheza Arsenal.Natumaini utalipokea ombi langu na kunileta Emirates na labda kujiunga na kikosi cha vijana ama kile cha wakubwa.Na baada ya miaka kadhaa naamini nitakulipa fadhira kwa kuniamini.
Asante.
0 comments:
Post a Comment