Barcelona,Hispania.
Barcelona imeendelea kujikita kileleni mwa ligi ya La Liga baada ya kuinyuka Celta Vigo kwa mabao 6-1 katika mchezo mkali na wa kusisimua uliopigwa katika uwanja wa Nou Camp.
Barcelona imepata mabao yake kupitia kwa Louis Suarez aliyefunga mara tatu,Lionel Messi,Neymar Jr na Ivan Rakitic huku John Guidetti akiipatia Celta Vigo bao la kufutia machozi kwa mkwaju wa penati uliopatikana baada ya kufanyiwa madhambi na mlinzi kulia wa Barcelona Jordi Alba.
Kufuatia ushindi huo Barcelona imeendelea kujikita kileleni baada ya kufikisha pointi 57 huku Atletico Madrid ikiwa na pointi 54 katika nafasi ya pili na katika nafasi ya tatu iko Real Madrid yenye pointi 53.
0 comments:
Post a Comment