Gijon,Hispania.
FC Barcelona imeendelea kujichimbia kileleni mwa ligi daraja la kwanza nchini Hispani [La Liga] baada ya usiku wa leo kuilaza Sporting Gijon kwa jumla ya mabao 3-1 katika mchezo mkali wa kiporo uliopigwa katika dimba la El Molinon,Gijon.
Nahodha Lionel Messi alianza kuifungia bao FC Barcelona la kuongoza dakika ya 25 kisha kuongeza jingine dakika ya 31huku Louis Suarez akifunga la tatu dakika ya 67 hii ikiwa ni baada ya kukosa bao la wazi baada ya Messi kuamua kumpasia penati badala ya kupiga moja kwa moja.Gijon imepata bao lake kupitia kwa Carlos Castro Garcia.
Mabao hayo mawili yamemfanya Messi kufikisha jumla ya mabao 301 na kuwa mchezaji wa kwanza kufikisha idadi hiyo ya mabao katika historia ya ligi ya La Liga.Mabao 50 zaidi ya nyota wa zamani wa Athletic Bilbao Telo Zarra (Aliyetamba miaka ya 1940s na 1950s) na mabao 55 zaidi ya Cristiano Ronaldo.
Kufuatia ushindi huo FC Barcelona imefikisha pointi 60 baada ya kushuka dimbani mara 24,pointi 6 zaidi ya Atletico Madrid iliyo katika nafasi ya pili na pointi 7 zaidi ya Real Madrid iliyo katika nafasi ya tatu.
0 comments:
Post a Comment