728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, February 27, 2016

    KUELEKEA MCHEZO WA JUMAPILI DHIDI YA ARSENAL,VAN GAAL AJA NA GOOD NEWS KUHUSU DE GEA.

    Manchester,England.

    Kocha wa Manchester United Louis van Gaal anaamini mlinda mlango namba moja wa klabu hiyo David De Gea atakuwa langoni kuivaana Arsenal jumapili hii katika mchezo wa ligi kuu England baada ya kukosa michezo mitatu kutokana na kuwa majeruhi.

    De Gea alipata jeraha la misuli siku nane zilizopita wakati akipasha moto mwili na kupelekea kukosa mchezo wa kwanza wa michuano ya Europa Ligi ambapo Manchester United ilichapwa na Midtjylland kwa jumla ya mabao 2-1.

    Wakati De Gea akitarajiwa kucheza dhidi ya Arsenal hali ya mlinzi Chris Smalling bado inatia shaka lakini Van Gaal amedokeza kuwa lolote linaweza kutokea katika mchezo huo wa kesho utakaopigwa katika dimba la Old Trafford.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KUELEKEA MCHEZO WA JUMAPILI DHIDI YA ARSENAL,VAN GAAL AJA NA GOOD NEWS KUHUSU DE GEA. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top