728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, February 10, 2016

    BARCELONA YAACHA NYOTA 11 MCHEZO COPA DEL REY DHIDI YA VALENCIA LEO

    Barcelona,Hispania.


    Klabu ya FC Barcelona imesafiri kwenda kuivaa Valencia katika mchezo wa marudiano wa kombe la Copa Del Rey bila ya nyota wake 11 walioiwezesha kuibuka na ushindi wa mabao 7-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa wiki iliyopita katika dimba la Nou Camp.

    Kocha mkuu wa klabu hiyo Luis Enrique amefikia uamuzi huo kutokana na FC Barcelona kuwa na michezo migumu katika mwezi huu wa Februari.Februari 23 FC Barcelona itavaana na Arsenal katika michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya kisha michezo ya ligi ya La Liga dhidi ya Celta Vigo, Sporting Gijon, Las Palmas na Sevilla.

    Nyota watakaokosekana kwenye mchezo wa leo ni:Claudio Bravo, Gerard Pique, Sergio Busquets, Dani Alves, Arda Turan, Andres Iniesta, Javier Mascherano, Jordi Alba, Luis Suárez, Lionel Messi na Neymar.

    Kikosi kilichosafiri ni:Marc Andre Ter Stegen, Jordi Masip, Douglas, Ivan Rakitic, Marc Bartra, Munir, Sandro Ramirez, Sergi Roberto, Adriano, Aleix Vidal, Thomas Vermaelen, Jereym Mathieu, Wilfrid Kaptoum, Sergi Samper, Dani Romera, Juan Camara Gerard Gumbauand Carles Aleña.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BARCELONA YAACHA NYOTA 11 MCHEZO COPA DEL REY DHIDI YA VALENCIA LEO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top