Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetuma salamu za
rambirambi kwa familia ya mwandishi wa habari za michezo nchini Hamis
Dambaya kufuatia kufiwa na mkewe, mwanae pamoja mama mkwe wake.
Katika salamu hizo, TFF imempa pole Dambaya kwa msibu huo mzito
uliomfika na kusema kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini,
Shirikisho liko pamoja nao katika kipindi hichi kigumu cha maombelzo ya
misiba hiyo.
Mkewe Hamis Dambaya, mwanane na mama mkwe wake wamefariki katika
ajali ya bus la Simba Mtoto iliyotokea leo asubuhi katikati ya eneo na
Muheza na Hale wakati wakiwa safarini kuelekea jijini Dar es salaam
wakitokea mkoani Tanga.
0 comments:
Post a Comment