Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko
taarifa ya kupigwa kwa mwandishi wa habari za michezo wa gazeti la
Mwanaspoti nchini, Mwanahiba Richard na kiungo wa timu ya Simba SC Mwiny
Kazimoto mjini Shinyanga.
Kufuatia kitendo hicho kilichotokea wakati wa mazoezi, TFF imesema
tukio liliofanywa na mchezaji huyo ni kinyume na sheria, taratibu/kanuni
zinazoendesha mpira wa miguu nchini, hivyo wanakilaani kitendo hicho
kwa nguvu zote.
Kwa kuwa tukio lilitokea wakati wa mazoezi, mpaka sasa TFF bado haijapokea taarifa rasmi kuhusiana na suala hilo.
0 comments:
Post a Comment