Kiev,Ukraine.
Manchester City imejiweka katika mazingira mazuri ya kusonga mbele hadi hatua ya robo fainali ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya baada ya kuichapa Dynamo Kiev kwa mabao 3-1 ikiwa ugenini jijini Kiev katika dimba la Olimpiyskiy.
Manchester City imejipatia magoli yake kupitia kwa Sergio Aguero,David Silva na Yaya Toure huku Vitaliy Buyalsky akiifungia Dynamo Kiev goli la kufutia machozi.
Timu hizo zitarudiana tena wiki mbili zijazo katika dimba la Etihad jijini Manchester United na mshindi atatinga hatua ya nane bora/robo fainali.
0 comments:
Post a Comment