London,England.
Arsenal imefufua matumaini ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu England baada ya leo hii kuitandika Leceister City kwa mabao 2-1 katika mchezo mkali uliopigwa katika dimba la Emirates,London.
Arsenal ambayo ilikuwa nyuma kipindi cha kwanza baada ya Jammie Vardy kuifungia Leceister City goli dakika ya 44 kwa mkaju wa penati iliamka na kusawazisha kupitia kwa Theo Walcott dakika ya 69 kisha kuongeza la pili dakika ya 95 kupitia kwa Danny Welbeck akiunganisha kwa kichwa mpira wa faulo wa Mesut Ozil.
Kufuatia ushindi huo Arsenal imefikisha pointi 51 pointi 2 nyuma ya Leceister City yenye pointi 53
Vikosi
Cech | Schmeichel | ||||||
Bellerin | Simpson | ||||||
Mertesacker | Morgan | ||||||
Koscielny | Huth | ||||||
Monreal | Fuchs | ||||||
Coquelin | Mahrez | ||||||
Ramsey | Drinkwater | ||||||
Oxlade-Chamberlain | Kante | ||||||
Ozil | Albrighton | ||||||
Sanchez | Okazaki | ||||||
Giroud | Vardy |
0 comments:
Post a Comment