Paris,Ufaransa.
Michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora ilianza kutimua vumbi lake jana jumanne kwa michezo miwili kupigwa katika miji ya Paris,Ufaransa na Lisbon,Ureno.
Katika mchezo uliopigwa huko Paris katika dimba la Parc des Princes mshambuliaji asiye na nafasi kikosi cha kwanza Edinson Cavani aliibuka shujaa baada ya kuifungia PSG bao dakika ya 78 na kufanya matokeo kuwa 2-1.
Cavani akitokea benchi dakika ya 74 aliitumia vyema pasi ya winga Angel Di Maria na kuipatia bao PSG baada ya kumpiga topo Thibaut Courtois kabla ya hapo matokeo yalikuwa 1-1.Zlatan Ibrahimovic akiifungia PSG bao la kuongoza dakika ya 39 kwa mpira wa adhabu kabla ya John Obi Mikel akiifungia Chelsea bao la kusawazisha dakika ya 45 akiunganisha kona ya Willian.
Katika mchezo uliopigwa huko Lisbon wenyeji Benfica wameitandika Zenit St. Petersburg kwa jumla ya bao 1-0 shukrani kwa Straika Mbrazil Jonas aliyetumia uzembe wa walinzi na kufunga.Michezo ya marudiano itapigwa Machi 9.
0 comments:
Post a Comment