London,England.
Kocha wa muda wa Chelsea Mdachi Guus Hiddink amelazimika kuwajumuisha makinda Matt Miazga na Jake Clarke-Salter katika kikosi cha wachezaji 20 kilichosafiri kwenda Ufaransa kuvaana na Paris Saint-
Germain katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano wa ligi ya mabingwa Ulaya huko Parc des Prince.
Hiddink amefikia uamuzi huo baada ya walinzi wake wa kati John Terry na Kurt Zouma kuwa majeruhi na hivyo kubaki na walinzi Gary Cahill pamoja na Branislav Ivanovic pekee katika nafasi hiyo.
Mbali ya Terry na Zouma Chelsea pia itazikosa huduma za kiungo wake Nemanja Matic ambaye anakabiliwa na adhabu ya kukosa mchezo mmoja huku Oscar akitarajiwa kucheza mchezo wa leo baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yanamkabili.
KIKOSI KAMILI
Makipa: Asmir Begovic, Jamal Blackman, Thibaut Courtois.
Walinzi: Cesar Azpilicueta, Gary Cahill,Jake Clarke-Salter, Branislav Ivanovic,
Matt Miazga, Baba Rahman
Viungo: Cesc Fabregas, Eden Hazard,Kenedy, Ruben Loftus-Cheek, John Mikel
Obi, Oscar, Pedro, Bertrand Traore, Willian
Mastraika: Diego Costa, Loic Remy
0 comments:
Post a Comment