Claudio Ranieri amesema kutolewa kwa Simpson kumeigharimu Leicester City lakini vinginevyo ushindi ulikuwa wao leo
Meneja wa Leicester City Claudio Ranieri anaamini uamuzi wa mwamuzi Martin Atkinson kumtoa Danny Simpson kwa kadi nyekundu Arsenal ikishinda 2-1 Jumapili ulisababisha mazingira magumu sana kwa timu yake kwa faulo ya kawaida.
Meneja huyo anaamini timu yake ingeshinda mechi hiyo katika uwanja wa Emirates kama wangecheza wachezaji 11 hadi dakika ya mwisho.
Jamie Vardy aliwapatia Mbweha hao goli la kuongoza kabla ya mapumziko kwa mkwaju wa penalti.. Hata hivyo Arsenal waliweza kurejea kwa nguvu kwa ushindi wa mabao kutoka kwa Theo Walcott na Danny Welbeck baada ya Leicester kupungua hadi watu 10 mnamo dakika ya 54 kufuatia kutolewa kwa Simpson.
"Ilikuwa ni mechi nzuri, yenye kasi. Sidhani kwa mechi ya kawaida kadi mbili za njano zilistahili kutolewa. Zilikuwa ni faulo za kawaida, lakini si za kadi ya njano. Nadhani mwamuzi alifanya maamuzi mabaya kumtoa Simpson. 11 dhidi ya 11 tungeshinda mechi. Mechi ilijawa na faulo nyingi, kwanini mchezaji atolewe? Namna gani," Meneja huyo wa Kiitaliano alikiambia BBC baada ya mechi.
"Tunajua kwamba Arsenal ni timu bora, wanakimbia na mpira kwa kasi na ni mahiri sana, lakini tulihitaji kujitahidi pia. Tulijaribu kufanya mashambulizi ya kushitukiza na tulimiliki mpira vizuri."
Lakini Ranieri amewapongeza Arsenal kwa ushindi, bado Leicester wanaongoza ligi.
"Bado tupo kileleni mwa msimamo, tunawazidi pointi mbili - lazima tuendelee kutabasamu. Tumepoteza kwa wapinzani wetu - hatuna budi kusema wamefanya kazi nzuri."CHANZO GOAL.COM
0 comments:
Post a Comment