Marseille, Ufaransa.
Abou Diaby anatarajia kuichezea mchezo wa kwanza klabu yake mpya ya Marseille leo katika mchezo hatua ya 16 bora ya kombe la Coupe de France dhidi ya Trelissac.
Diaby ambaye amekuwa nje ya uwanja kutokana na kuwa majeruhi kwa siku 506 tangu aichezee Arsenal Septemba 2014 katika michuano ya kombe la ligi kabla ya kutupiwa virago mwezi Juni mwaka jana na kutua Marseille amejumuishwa katika kikosi cha wachezaji 19 kilichosafiri kwenda Bordeaux kuivaa Trelissac inayoshiriki ligi daraja la nne.
0 comments:
Post a Comment