Cairo,Misri.
Vinara wa ligi kuu ya Misri klabu ya Al Ahly leo wamemtangaza Mdachi Martin Jol kuwa Kocha wao mpya.
Jol aliyewahi kuvinoa vilabu vya Tottenham, Hamburg, Ajax na Fulham amechukua nafasi hiyo toka kwa Zizo aliyekuwa akihudumu kama kocha wa muda baada ya Mreno Jose Peseiro kutimkia Porto.
Ujio wa Jol katika klabu ya Al Ahly umekuja siku moja tu tangu Alex McLeish ajiunge na Zamalek iliyo nyuma ya Al Ahly kwa pointi tatu.
0 comments:
Post a Comment