728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, February 12, 2016

    MESSI AMALIZA GUNDU LA LIGA

    Barcelona,Hispania.


    Hatimaye Lionel Messi amemaliza gundu la muda mrefu baada ya leo hii kutwaa kwa mara ya kwanza tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa ligi ya La Liga kwa mwezi Januari.Messi mshindi wa tuzo tano za mchezaji bora wa dunia {Ballon d' Or} kabla ya leo hakuwahi kutwaa tuzo hiyo ambayo hutolewa kwa mchezaji aliyefanya vizuri katika mwezi husika.

    Messi ametwaa tuzo hiyo akiwashinda Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Diego Godin wa Atletico Madrid baada ya kufunga mabao sita katika michezo mitano ya La Liga.Tuzo ya mchezaji bora wa mwezi ilianza kutolewa mwaka 2013 na mpaka kufikia leo jumla ya wachezaji 17 wameshaitwaa huku Cristiano Ronaldo na Diego Godin wakiwa vinara baada ya kutwaa mara mbili kila mmoja.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MESSI AMALIZA GUNDU LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top