728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, February 25, 2016

    KISA MASCHERANO!!CHAMBERLAIN NJE ARSENAL,HATI HATI KUKOSA MICHUANO YA EURO

    London,England.

    Winga wa Arsenal Muingereza Alex Oxlade-Chamberlain huenda akakaa nje ya uwanja kwa kipindi kisichojulikana kufuatia jeraha la goti na kifundo mguu alilolipata baada ya kugongana na kiungo wa FC Barcelona Muargentina Javier Mascherano siku ya jumanne katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora wa klabu bingwa Ulaya na Arsenal kulala 2-0 nyumbani Emirates.

    Siku ya jana jumatano Chamberlain,22 alifanyiwa vipimo na leo alhamis taarifa rasmi itatolewa juu ya ukubwa wa tatizo lake ambapo taarifa za awali zinadai huenda akawa nje mpaka mwishoni mwa mwezi Machi na hivyo kuwa na nafasi finyu ya kuwepo katika kikosi cha Uingereza kitakachosafiri kwenda Ufaransa katika michuano ijayo ya Ulaya itakayoanza kutimua vumbi lake mwezi Juni na kuisha Julai.

    Chamberlain alipata jeraha hilo baada ya kugongana vibaya na Mascherano wakati akijaribu kulikalibia lango la FC Barcelona kwa kasi na kulazimika kutolewa uwanjani na nafasi yake kuchukuliwa na Theo Walcott.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KISA MASCHERANO!!CHAMBERLAIN NJE ARSENAL,HATI HATI KUKOSA MICHUANO YA EURO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top