London,England.
Arsenal inafikiria kumpiga bei winga wake Muingereza Alex Oxlade-Chamberlain wakati wa dirisha lijalo la usajili barani Ulaya.
Habari za kuamini zilizoifikia Soka Extra zinadai kuwa Arsenal imefikia uamuzi huo baada ya winga huyo mwenye miaka 22 kushindwa kufikia matarajio ya benchi la ufundi la klabu hiyo ya kaskazini mwa London.
Chamberlain alijiunga na Arsenal mwaka 2011akiwa na miaka 17 akitokea Southampton kwa dau la £12m.Mpaka sasa Chamberlain amefanikiwa kuichezea Arsenal michezo 149 katika michuano yote.
Arsenal itamuuza Chamberlain kwenda klabu yoyote ikiwa itapokea ofa ya kati ya £15 na kuendelea
0 comments:
Post a Comment