Kigali,Rwanda.
APR ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Amahoro jijini Kigali, leo imeitandika Mbabane kutoka Swaziland kwa mabao 4-0 katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ya awali.
Kwa ushindi huo, maana yake APR imesonga mbele kwa jumla ya mabao 4-1 na sasa hakuna ubishi tena ndiyo itakayokutana na mabingwa wa Tanzania Yanga katika raundi inayofuata.
Yanga imeishinda Cercle de Joachim ya Mauritius kwa mabao 2-0 leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,hivyo kusonga mbele kwa jumla ya mabao 3-0 baada ya ushindi wa bao 1-0 katika mechi ya kwanza ugenini.
Kwa upande wa APR, shukurani kubwa kwa beki wake Abdul Rwatubyaye aliyepiha hat trick katika mechi hiyo ambayo APR walionekana kutakata.
CHANZO:SALEH JEMBE
0 comments:
Post a Comment