Ligi Daraja la Kwanza (StarTimes League) inatarajiwa kumalizika
wikiendi hii kwa michezo 12 kuchezwa kwa wakati mmoja katika viwanja
mbalimbali nchini, huku Kundi A na C zikisaka vinara watakaopnda Ligi
Kuu msimu ujao.
Bodi ya Ligi (TPLB) imeviandikia barua vilabu vyote vinavyoshiriki
Ligi hiyo, wasimamizi wa vituo kuwafahamisha kuwa mechi zote zinatakiwa
kuchezwa kwa muda mmoja na kusisitiza kuwa mechi zote zitaanza saa 10
kamili jioni bila kujali kama jua linawahi au kuchelewa kuzama.
Ni jukumu la Msimamizi na Kamishna kuhakikisha mechi yake inaanza
katika muda uliotajwa (saa 10 kamili) bila kukosa. Utekelezaji wa
maelekezo haya ni muhimu ikiwa ni moja ya njia ya kukabiliana na vitendo
vyovyote vya upangaji wa matokeo vinavyoweza kujitokeza.
Mechi za mwisho za Kundi A hatua ya kwanza ya Ligi ya Daraja la
Kwanza ya StarTimes kati ya Friends Rangers FC vs Kiluvya United FC
(Mabatini), Polisi Dar vs Polisi Dodoma (Shirika la Elimu Kibaha),
Ashanti United vs African Lyon (Karume) na Mji Mkuu vs Kinondoni
Municipal Council FC zitachezwa Februari 14, 2016 katika viwanja husika.
Mechi za mwisho za Kundi B hatua ya kwanza ya Ligi ya Daraja la
Kwanza ya StarTimes kati ya Kimondo Super SC vs Kurugenzi FC (Vwawa),
Njombe Mji vs Lipuli FC (Amani), Ruvu Shooting vs Polisi Morogoro
(Mabatini) na Burkina FC vs JKT Mlale (Jamhuri) zitachezwa Februari 13,
2016.
Mechi za mwisho za Kundi C hatua ya kwanza ya Ligi ya Daraja la
Kwanza ya StarTimes kati ya Mbao FC vs Polisi Mara (CCM Kirumba), Polisi
Tabora vs JKT Oljoro (Ali Hassani Mwinyi) na JKT Kanembwa vs Geita Gold
(Lake Tanganyika) zitachezwa Februari 13, 2016 katika viwanja husika.
0 comments:
Post a Comment