728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, February 26, 2016

    SUNDAY OLISEH ABWAGA MANYANGA KUIFUNDISHA SUPER EAGLES

    .Lagos,Nigeria.

    Sunday Oliseh ametangaza kubwaga manyanga kuifundisha timu ya taifa ya Nigeria maarufu kama Super Eagles.

    Oliseh ambaye alianza kuinoa timu hiyo Julai 2015 ametangaza kubwaga manyanga asubuhi ya leo ijumaa kupitia ukurasa wake wa rasmi wa Twitter [@SundayOOliseh] baada ya kuwa katika mvutano wa muda mrefu na chama cha soka cha Nigeria NFF.

    Oliseh ameelewa kuwa kukosa kuungwa mkono,kutolipwa mshahara kwa wakati,wachezaji na wasaidizi wake kuburuzwa na kutothaminiwa kwa benchi zima la ufundi ni baadhi tu ya sababu zilizofanya afikie uamuzi huo.

    Kwa kumalizia Oliseh ameshukuru kwa kupata nafasi ya kucheza,kuwa nahodha na mwisho kupata fursa ya kuifundisha Nigeria.

    .
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SUNDAY OLISEH ABWAGA MANYANGA KUIFUNDISHA SUPER EAGLES Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top