Madrid,Hispania.
Staa wa Real Madrid Mreno Cristiano Ronaldo amesema kwasasa hafikirii kuachana na klabu hiyo lakini mpango huo unaweza kuja mwaka 2018 pindi mkataba wake wa sasa na miamba hiyo ya La Liga utakapokuwa umefikia tamati.
Ronaldo ambaye wiki hii atakuwa anafikisha umri wa miaka 31 ameyasema hayo jana jumatatu baada ya kukabidhiwa tuzo ya mfungaji bora wa La Liga iitwayo Pichichi baada msimu uliopita kuongoza chati za ufungaji kwa kufunga magoli 48.
Amesema "Nataka kubaki hapa [Real Madrid] kwa miaka miwili yani mwaka 2018 pindi mkataba wangu utakapokuwa umefikia mwisho.Siendi popote hivi karibuni,Napenda kucheza hapa na La Liga ndiyo ligi bora zaidi."
Kauli hiyo ya Ronaldo imekuja baada ya uvumi kuenea kuwa staa huyo anafikiria kuachana na Real Madrid na kujiunga na Paris Saint Germain ama klabu yake ya zamani ya Manchester United.
0 comments:
Post a Comment