728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, February 10, 2016

    HII NDIYO KAULI YA SAID NDEMLA BAADA YA KUENDELEA KUKAA BENCHI SIMBA



    KIUNGO wa Simba, Said Ndemla, amesema haumii kichwa, licha ya kutopata nafasi kwenye kikosi cha kwanza mara kwa mara, kwa sababu anaamini anao uwezo wa kucheza nafasi nyingi kwenye kikosi hicho cha Mganda, Jackson Mayanja. 

    Ndemla alisema anamudu kucheza kiungo namba sita na nane, winga ya kulia na kushoto, hata mshambuliaji msaidizi, yaani namba 10, hivyo ana nafasi kubwa ya kurejea kikosi cha kwanza.
     
    “Sijui kwa nini kocha hanitumii, yeye ndiye anayejua mahitaji ya kikosi chake, sihitaji kumuingilia katika hilo, ila kwa upande wangu nina imani nitarejea kwenye kikosi,” alisema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HII NDIYO KAULI YA SAID NDEMLA BAADA YA KUENDELEA KUKAA BENCHI SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top