Ligi Daraja la Pili (SDL) inatarajiwa kumalizika wikiendi hii kwa
michezo 12 kuchezwa katika makundi ya A, B, C & D katika viwanja
mbalimbali nchini, huku kila kundi likitoa timu moja ya juu itakayocheza
fainali za kupanda ligi daraja la kwanza msimu ujao.
Leo Ijumaa, michezo mitatu ya kundi C itachezwa katika raundi hiyo
ya mwisho, Villa Squad watacheza dhidi ya Mshikamano (Mabatini,
Mlandizi), Abajalo Dar v Karikaoo FC (Karume) na Changanyikeni watakuwa
wenyeji wa Cosmopolitan katika uwanja wa Shirika la Elimu Kibaha.
Kundi A, Jumamosi Green Warriors watawakaribisha Abajaro Tabora
katika uwanja wa Mabatini Mlandizi, Transit Camp watakua wenyeji wa
Mvuvumwa uwanja wa Kambarage Shinyanga, huku siku ya Alhamis Singida
United watacheza dhidi ya Mirambo uwanja wa Namfua mjini Singida.
Jumamosi Kundi C, Alliance Schools watakua wneyeji wa Bulyankulu
katika uwanja wa CCM Kirumba, JKT Rwamkoma watacheza dhidi ya Pamba FC
uwanja wa Karume Musoma, na Madini FC watakua wenyeji wa AFC Arusha
uwanja wa Mbulu.
Kundi D, Jumapili Mkamba Rangers watacheza dhidi ya Wenda FC uwanja
wa CCM Mkamba, Sabasaba watakua wenyeji wa The Mighty Elephant uwanja wa
Jamhuri mjini Morogoro, huku Mbeya Warriors wakicheza dhidi ya African
Wanderes katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Timu moja ya kwanza kutoka katika kila kundi zitacheza hatua ya
Fainali Machi 7-14, 2015 uwanja wa Karume jijini Dar es salaam, ili
kupata timu tatu za juu zitakazopanda moja kwa moja ligi daraja la
kwanza (StarTimes League) msimu ujao.
Kupata msiammo wa Ligi Daraja la Pili (SDL) fuata link hii http://tff.or.tz/league/tff-league/18-second-division-league
0 comments:
Post a Comment