Lubumbashi,Congo.
Mabingwa wa ligi ya mabingwa Afrika TP Mazembe inayochezewa na Mtanzania Thomas Ulimwengu leo jioni itashuka katika dimba lake la nyumbani kuwania taji la nne la Super Cup pale itakapovaana na mabingwa wa shirikisho Etoile du Sahel ya Tunisia.
TP Mazembe ambao ni mabingwa wa taji hilo mara mbili baada ya kulitwaa mwaka 2010 na 2011 ushindi wowote leo hii utawawezesha kutwaa taji hilo kubwa kwa ngazi ya vilabu Afrika kwa mara ya tatu.
Ndoto hiyo ya TP Mazembe huenda isitimie kirahisi kutokana na ukweli kwamba Etoile du Sahel siyo timu ya kuibeza kwani tayari ina mataji mawili ya Super Cup iliyoyatwaa mwaka 1998 na 2008.
0 comments:
Post a Comment