London,England.
Traore akiifungia Chelsea goli la tano
Traore akiifungia Chelsea goli la tano
Betrand Traore ameandika historia ya kuwa mchezaji wa kwanza toka taifa la Burkina Faso kufunga goli katika mchezo wa ligi kuu nchini England baada ya kuifungia Chelsea goli moja katika ushindi wa magoli 5-1 dhidi ya Newcastle United jana jumamosi.
Traore,19 ambaye aliingiwa uwanjani akitokea benchi kuchukua nafasi ya Diego Costa alifunga goli hilo dakika ya 83 ya mchezo akimalizia krosi safi ya mlinzi wa kulia Cesar Azpilicuta.Mpaka sasa wachezaji toka mataifa 94 wamefanikiwa kufunga magoli katika michezo mbalimbali ya ligim kuu nchini England tangu kuasisiwa kwake mwaka 1992.
Yafuatayo ni mataifa ambayo wachezaji wake bado hawajawahi kufunga goli katika ligi kuu ya England.....Pakistan,Zambia,Albania,Bolvia,Cape Velde,Cyprus,Gambia,Visiwa vya Faroe,Malta,Oman,Lithuania,Guadeloupe,Mauritius na Guinea-Bissau.
Albania,
Bolivia, Cape Verde Islands, Cyprus, Estonia, Faroe Islands, Gambia,
Guadeloupe, Guinea-Bissau, Lithuania, Malta, Oman, Pakistan, Seychelles,
Zambia - See more at:
http://www2.premierleague.com/en-gb/news/news/2015-16/feb/140216-matchweek26-chelsea-vs-newcastle-post-match-stats.html#sthash.LeyLIR39.dpuf
Bertrand Traore
0 comments:
Post a Comment