728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, February 27, 2016

    REAL MADRID YATOTA NYUMBANI YANYUKWA 1-0 NA ATLETICO MADRID

    Madrid,Hispania.

    Real Madrid imeshindwa kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani wa Santiago Bernabeu baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 toka kwa mahasimu wao wa jiji la Madrid Atletico Madrid.

    Bao pekee la mchezo huo limetiwa kimiani dakika ya 53 na mshambuliaji Mfaransa Antonio Griezmann akimalizia pasi ya mlinzi Felipe Luiz aliyepanda kusaidia mashambulizi

    Kufuatia matokeo hayo Atletico Madrid imeendelea kung'ang'ania nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ya La Liga baada ya kufikisha pointi 58 ikiiacha Real Madrid katika nafasi ya tatu na pointi zake 54.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: REAL MADRID YATOTA NYUMBANI YANYUKWA 1-0 NA ATLETICO MADRID Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top