Marekani.
Kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo ya Nike imetangaza kuvunja mkataba wa kibiashara na bondia Manny Pacquiao ukiwa ni muda mfupi tangu bondia huyo awafananishe watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja na wanyama.
Nike ambayo imekuwa ikifanya biashara na Manny Pacquiao tangu mwaka 2006 imefikia uamuzi huo baada ya majuzi bondia huyo kupinga hadharani ushoga/usagaji na kudiriki kusema watu wanaojihusisha na vitendo hiyo ni wabaya kuliko wanyama.
Pacquiao aliitoa kauli hiyo katika mahojiano maalumu aliyoyafanya na kituo cha luninga cha TV5 cha nyumbani kwao Ufilipino.Japo baadae Pacquiao aliomba radhi kwa kauli hiyo lakini Nike kupitia mtandao wake imeripoti kuwa imechukizwa na kauli hiyo na kuamua kuvunja mkataba nae mkataba huku ikisisitiza kuwa haiungi mkono vitendo vyovyote vile kwa kiubaguzi kwa jamii zote za watu.
0 comments:
Post a Comment