728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, February 11, 2016

    BARCA YATINGA FAINALI COPA DEL REY,YATOKA SARE NA VALENCIA,YAWEKA REKODI MPYA

    Barcelona,Hispania.

    Sare ya bao 1-1 iliyoipata FC Barcelona dhidi ya Valencia jana usiku katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya kombe la Copa del Rey siyo kwamba imeiwezesha kutinga fainali ya michuano hiyo pekee bali pia imeiwezesha miamba hiyo ya Catalunya kuweka rekodi ya kucheza michezo 29 bila kupoteza mchezo hata mmoja katika michuano yote na kuvunja rekodi yake ya mwaka 2010/11 ya kucheza michezo 28 bila kupoteza.

    Bao la kusawazisha lililofungwa dakika za mwisho na kiungo kinda Mcameroon Wilfred Kaptoum liliinyima Valencia ushindi baada ya kuongoza kwa bao la Alvaro Negredo.

    Kufuatia ushindi huo FC Barcelona imefanikiwa kutinga fainali ya Copa del Rey kwa jumla ya mabao 8-1.Hii ni mara ya tano kwa FC Barcelona kutinga fainali ndani ya miaka sita na huenda ikavaana na Sevilla Mei 21 ambayo leo itakuwa ikicheza na Celta Vigo.Katika mchezo wa kwanza Sevilla iliichapa Celta Vigo kwa mabao 4-0.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BARCA YATINGA FAINALI COPA DEL REY,YATOKA SARE NA VALENCIA,YAWEKA REKODI MPYA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top