GENEVA,USWISI.
Kamati ya nidhamu ya shirikisho la vyama vya soka duniani FIFA leo limemfungia aliyekuwa katibu wake mkuu Jerome Valcke kutojihusisha na masuala ya soka kwa kipindi cha miaka 12 baada ya kumkuta na hatia ya matumizi wabaya ya madaraka.
Valcker ambaye ni mshirika wa karibu wa Sepp Blatter amekutwa na hatia ya kutumia ndege ya shirikisho hilo kwa mambo binasfi,kuomba na kupokea rushwa pamoja na kuharibu ushahidi wa makosa yaliyokuwa yakimkabili.
Mbali ya kifungo hicho pia Valcker ametozwa faini ya pesa za Kiswisi 100,000 ambazo ni sawa na dola 102,500.
0 comments:
Post a Comment