Barcelona,Hispania.
Msimu ujao Barcelona huenda ikaanza kudhaminiwa na kampuni ya vinywaji baridi ya Pepsi na kuachana moja kwa moja na mdamini wake wa sasa shirika la usafiri wa anga la Qatar Airways baada ya shirika hilo lenye makao makuu yake huko Doha,Qatar kudaiwa kuleta dharau kwa miamba hiyo ya Hispania.
Mapema wiki iliyopita iliripotiwa kuwa vigogo wa Barcelona walifika Doha,Qatar kuonana na wakuu wa Shirika hilo kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kusaini mkataba mpya lakini walikwama baada ya wenyeji wao kugoma kukutana nao kutokana na kutokuwa na mahusiano ya mazuri siku za hivi karibuni.
Taarifa za kuaminika zinasema kuwa kutokana na mgongano huo kampuni ya Pepsi imefungua mazungumzo na Barcelona na iko tayari kuidhamini miamba hiyo kwa kipindi cha miaka mitano huku ikiilipa kitata cha Dola 70m kwa mwaka kwa kuvaa jezi yenye nembo ya Pepsi kifuani.
0 comments:
Post a Comment