Leceister,England.
Leicester City imeshindwa kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani wa King Power baada ya kulazimishwa kwenda sare ya mabao 2-2 na West
Bromwich Albion.
Leicester City ambayo iko kileleni mwa ligi kuu England imejipatia mabao yake kupitia kwa Danny
Drinkwater na Andy King huku wageni West
Bromwich Albion wakifunga kupitia kwa Salomon Rondon na Craig Gardener aliyefunga kwa mpira wa adhabu wa mita 25.
Kufuatia ushindi huo Leicester City imefikisha pointi 57 pointi 3 dhidi ya Tottenham Hotspurs ambayo leo jumatano itavaana na Westham United na iwapo itashinda itakaa kutokana na kuwa na wastani mzuri wa mabao.
Katika mchezo mwingine wa ligi kuu uliopigwa huko Carrow Road,Chelsea imechupa mpaka nafasi ya nane baada ya kuichapa Norwich City kwa mabao 2-1.
Shukrani za dhati ziende kwa mabao ya Diego Costa na kinda Mbrazil Kennedy aliyefunga sekunde ya 39 tu ya mchezo na bao hilo kuwa bao la mapema zaidi kufungwa msimu huu katika michezo ya ligi kuu England.
Matokeo mengine
Bournemouth 2-0 Southampton
Aston Villa 1-3 Everton
Sunderland 2-Crystal Palace
Ligi hiyo itaendelea tena leo kwa michezo mitano:Westham United itakuwa nyumbani kuvaana na Tottenham,Arsenal itakuwa mwenyeji wa Swansea City huko Anfield Liverpool itakuwa mwenyeji wa Manchester City,Manchester United dhidi ya Watford na Stoke dhidi ya Newcastle United.
0 comments:
Post a Comment