Kampala,Uganda.
Serikali ya Uganda imetangaza kuchukua jukumu la kugharamia usafiri pamoja na mazishi ya aliyekuwa mlinda mlango wa nchi hiyo Abel Dhaira aliyefariki siku ya jumapili huko Iceland alipokuwa akipatiwa matibabu ya Kansa.
Kwa mujibu wa baba mzazi wa merehemu Abel,aitwaye Bright Dhaira na msemaji wa serikali Lindah Nabusayi ni kwamba serikali imeamua kuchukua jukumu hilo ili kuenzi mchango wa nyota huyo kwa soka la Uganda.
Dhaira aligundulika kuwa na Kansa mwaka jana baada ya kufanyiwa vipimo katika hosptali ya Nsambya na hali ilipokuwa mbaya alipelekwa Iceland ambako alikuwa akitibiwa kwa gharama za klabu yake ya IBV Vestmanaeyjar.
0 comments:
Post a Comment