728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, March 24, 2016

    HUYU HAPA MBADALA WA ARBERTO MORENO LIVERPOOL

    Na Paul Manjale.

    Liverpool,England.

    Kwa mujibu wa Charlie Phillippe wa gazeti la 
    Express la England,Liverpool imeanza kumfukuzia mlinzi wa kushoto wa Shalke 04 Mbosnia Sead Kolasinac,22 ili kuchukua nafasi ya mlinzi Alberto Moreno anayetarajiwa kuuzwa katika majira yajayo ya kiangazi barani Ulaya.

    Taarifa za ndani zinadai kuwa Liverpool imefikia uamuzi wa kuachana na Moreno baada ya mlinzi huyo raia wa Hispania kushindwa kufanya kazi yake ya ulinzi barabara na badala yake amekuwa akishambulia zaidi hali ambayo hupelekea matatizo pindi Liverpool inaposhambuliwa.

    Nyota wa zamani wa Liverpool John Aldridge ameiita tabia hiyo ya Moreno kuwa ni hatari sana na kutaka atafutwe mlinzi mwingine ambaye atakuwa na utulivu katika eneo lake.

    Kolasinac ambaye pia ana uwezo wa kucheza kama kiungo wa ulinzi msimu huu ameichezea Shalke 04 jumla ya michezo 18 katika mashindano yote.

    Ili kuharakisha dili hilo Liverpool inatarajia kumtumia kocha wake Zeljko Buvac ambaye pia ni raia wa Bosnia kumshawishi Kolasinac amwage wino Anfield.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HUYU HAPA MBADALA WA ARBERTO MORENO LIVERPOOL Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top