Na Paul Manjale
London,England.
Arsenal huenda ikafanya usajili wa kushtukiza ndani ya masaa 48 yajayo baada ya kuripotiwa kushinda mbio za kuiwania saini ya kiungo kinda wa zamani wa Chelsea Mreno Domingos Quina,16.
Kutoka England habari zinadai kuwa Arsenal imevibwaga vilabu vya Manchester United na Tottenham ambavyo navyo vilikuwa vikimuwania kinda huyo aliyegoma kurejea Chelsea baada ya kushindwa kupenya na kuingia kikosi cha wakubwa.Mapema wiki iliyopita Quina alikaa kurejea Chelsea muda mfupi baada ya kikuchezea kikosi cha vijana cha Ureno.
Quina alijiunga na Chelsea mwaka 2012 baada ya kufanya vizuri katika kikosi cha watoto cha Benfica ya nyumbani kwao Ureno.
Wakati huo huo Arsenal itabidi isubiri mpaka mwakani ndipo iweze kumpa mkataba Quina kwani kwa mujibu wa sheria za England mchezaji anaruhusiwa kusaini mkataba baada ya kufikisha miaka 17 na siyo chini ya hapo.
0 comments:
Post a Comment