728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, March 30, 2016

    BAADA YA KUIONEA UJERUMANI UGENINI,ENGLAND YAANGUKIA PUA NYUMBANI YACHAPWA 2-1 NA UHOLANZI WEMBLEY.

    London,England.

    Baada ya kufuzu kwa mbwembwe michuano ya Ulaya (Euro 2016) pamoja na majuzi kuitandika Ujerumani kwa mabao 3-2 ugenini,England imeshindwa kujitutumia nyumbani baada ya jummanne usiku kukubali kichapo cha magoli 2-1 toka kwa Uholanzi katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki.

    Magoli yaliyoipa ushindi Uholanzi ugenini Wembley yamefunga dakika za 50 na 77 kupitia kwa Vincent Janssen aliyefunga kwa mkwaju wa penati baada ya Danny Rose wa England kunawa mpira katika eneo la hatari.

    Goli la pili limefungwa na Luciano Narsingh huku lile la Wenyeji England likifungwa dakika ya 41 na Jamie Vardy baada ya kumegewa pande zuri na mlinzi Kyle Walker aliyepanda kusaidia mashambulizi.

    Mchezo wa jana umekuwa wa kwanza kwa England kupoteza nyumani tangu walipofungwa mwaka 2013 na Ujerumani.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BAADA YA KUIONEA UJERUMANI UGENINI,ENGLAND YAANGUKIA PUA NYUMBANI YACHAPWA 2-1 NA UHOLANZI WEMBLEY. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top