Nairobi,Kenya.
Kenya imeendelea kuburuza mkia katika mbio za kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya Afrika hapo mwakani nchini Gabon baada ya leo hii kukubali kichapo cha 1-0 nyumbani Nyayo toka kwa Guinea Bissau.
Kenya ambayo iko Kundi E ilihitaji ushindi katika mchezo wa leo lakini bao la dakika ya 81 la Sanchez Semedo Cicero Casmiro lilitosha kufuta matumaini ya Kenya ambayo mpaka sasa imeshapoteza michezo mitatu huku ikifanikiwa kuvuna pointi moja pekee katika michezo minne.
FUJO
Mchezo uliingia dosari dakika za mwisho baada ya mashabiki wa Kenya kuzua vurugu wakipinga maamuzi ya mwamuzi matokeo yaliyopelekea polisi kuingilia kati na kuanza kulipua mabomu ya machozi.
0 comments:
Post a Comment