728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, March 26, 2016

    KUELEKEA AFCON 2017 ALGERIA KIBOKO YAPIGA MTU 7-1

    Na Paul Manjale.

    ALGIERS,ALGERIA

    Algeria imeendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa Kundi J baada ya jana ijumaa kuitandika Ethiopia kwa jumla ya mabao 7-1 katika mchezo safi wa kusaka tiketi ya kushiriki michuano ijayo ya AFCON.

    Ikicheza nyumbani katika dimba la Pustapha Tchaker huko Blida,Algeria ilipata mabao yao kupitia kwa Sofiane Feghoulii aliyefunga mara mbili dakika za 24 na 
    48),Islam Slimani naye alifunga mara mbili dakika za 32 na 90 huku mabao mengine yakifungwa na Taïder dakika ya 75) na Ghezzal dakika ya 81.

    Ethiopia ilipata bao la kufutia kupitia kwa mshambuliaji wake Getaneh Kebede dakika ya 85.

    Kufuatia matokeo hayo Algeria bado iko kileleni baada ya kujikusanyia pointi 9 huku Ethiopia ikiwa nafasi ya pili na pointi zake 4.

    Timu hizo zitarudiana tena Machi 29 jijini Addis Ababa,Ethiopia.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KUELEKEA AFCON 2017 ALGERIA KIBOKO YAPIGA MTU 7-1 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top