Leceister,England.
Kiungo anayetamba katika klabu ya Leceister City Danny Drinkwater amesema ugumu wa kupata namba katika kikosi cha kwanza cha Mancheter United ndiyo sababu iliyofanya aachane na miamba hiyo ya ligi kuu England.
Drinkwater, 26, ambaye ameitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha timu ya taifa ya England kinachojiandaa na michezo ya kirafiki dhidi ya Uholanzi na Ujerumani alijiunga na Leceister City mwaka 2012 baada ya kukaa Manchester United kwa kipindi cha miaka 13.
Kabla ya kutua Leceister City Drinkwater aliwahi kucheza kwa mkopo katika vilabu vya Huddersfield, Cardiff, Watford na Barnsley United.
0 comments:
Post a Comment