728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, March 26, 2016

    UFARANSA YAIPIGA UHOLANZI 3-2 UGENINI,DEPAY SAFI

    Amsterdam,Uholanzi.

    Timu ya taifa ya Ufaransa imeizidi ujanja timu ya taifa ya Uholanzi na kuitungua mabao 3-2 katika mchezo mkali wa kimataifa wa kirafiki uliopigwa jana usiku katika dimba la Amsterdam Arena,Uholanzi.

    Ufaransa ambao ni wenyeji wa michuano ya Ulaya itakayoanza kutimua vumbi lake Juni imepata mabao yake kupitia kwa Antoine Griezmann aliyefunga kwa mkwaju wa faulo,Olivier Giroud na Blaise Matuidi.

    Wenyeji Uholanzi wao walipata mabao yao kupitia kwa Luuk De Jong na Ibrahim Afellay kufuatia kazi nzuri ya winga Memphis Depay aliyepika mabao yote mawili.

    Mchezo huo wa jana usiku pia ulikuwa maalumu kwa ajili ya kutoa heshima kwa gwiji wa soka wa Uholanzi Johan Cruyff aliyefariki siku ya alhamisi kwa ugonjwa wa kansa.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: UFARANSA YAIPIGA UHOLANZI 3-2 UGENINI,DEPAY SAFI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top