Dier akishangilia goli la ushindi.
Na Paul Manjale.
Berlin,Ujerumani.
England imeonyesha kuwa itakuwa moto wa kuotea mbali katika fainali zijazo za Ulaya baada ya jumamosi usiku kutoka nyuma na kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya mahasimu wao wakubwa Ujerumani katika mchezo mkali wa kirafiki uliopigwa katika dimba la Olympiastadion huko Berlin.
England ambayo mpaka dakika ya 60 ilikuwa nyuma kwa magoli 2-0 ya Toni Kroos na Mario Gomez ya dakika za 41' na 57' ilifanikiwa kubadili matokeo kwa magoli ya dakika za 61,74 na 91 ya Harry Kane, Jamie Vardy na Eric Dier aliyefunga goli la ushindi ambalo pia ni goli lake la kwanza kufunga akiwa na jezi ya England.
England itashuka tena dimbani siku ya jumanne usiku huko Wembley kuumana na Uholanzi ambayo siku ya ijumaa ikiwa nyumbani ilichapwa mabao 3-2 na Ufaransa.
Chini ni uwanja wa Olympiastadion uliochezewa mchezo huo wa Ujerumani na England.
0 comments:
Post a Comment